STAA wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amefunguka kuwa, haogopi watu wanaomsema kwa ubaya kila kona bali anaangalia kile kilichomsababisha kuwa mwimbaji ambaye nyimbo zake zinawabariki wengi.

Rose aliliambia Wikienda kuwa, watu wamekuwa wakimzushia mambo mengi ya ajabu, lakini hawajui anachokifanya kwa sasa ila siku wakija kugundua wataumbuka ndiyo maana yupo kimya hata kwenye muziki huo hivyo wanaomsema na kumtakia mabaya anawaombea kila kukicha na Mungu atawalipa kila mmoja kwa wakati wake.

“Najua aliyeniita katika huduma ya uimbaji ni Mungu na siyo mwanadamu, hivyo kwa kila jambo namsikiliza yeye siyo mwanadamu mwenzangu, siogopi wanaonisema vibaya maana ninaamini aliyeniita hataniacha,” alisema Rose ambaye mara kwa mara amekuwa akiandikwa kwa stori za utapeli.
WAKATI yakisemwa mengi juu ya ujauzito alionao ambao kwa sasa hauhitaji miwani ili kuuona, mwanamitindo matata Bongo, Hamisa Mobeto amepasua jipu juu ya mimba hiyo kufuatia kutajwa kwa msanii wa Bongo Fleva.

Kwa siku kadhaa sasa, kumekuwa na habari nyingi juu ya Hamisa kudaiwa kubeba ujauzito wa jamaa huyo ilihali akijua msanii huyo ana mpenzi wake ambaye amekuwa akikwaruzana naye mara kwa mara.

HAMISA AJIFICHA
Ilielezwa kwamba, kufuatia maneno mengi juu ya jambo hilo, Hamisa amekuwa akijifi cha kukwepa vyombo vya habari, lakini Wikienda limefanikiwa kumbana na kufunguka mazito.


KWELI MJAMZITO
Hamisa ambaye wengi wamekuwa hawana uhakika kama kweli ni mjamzito, mbali na kukiri kuwa kweli ni mjamzito wa mtoto wa pili baada ya yule wa awali wa kike aliyezaa na bosi maarufu wa redio jijini Dar, aliliambia Wikienda kuwa, yanasemwa mengi juu ya mimba yake hasa aliyempachika lakini yeye hajali kwani yupo tayari kupokea matusi ya jumla na rejareja.

Wikienda: Je, ni kweli mimba ni ya msanii wa Bongo Fleva kama inavyosemekana?
Hamisa: Siko tayari kusema ujauzito ni wa nani. Watu waelewe hivyohivyo wanavyoelewa.

Wikienda: Lakini kila mtu anajua ni wa msanii huyo, je, ni kweli?
Hamisa: Wanaomtaja baba wa ujauzito wangu hawanisumbui kabisa na wakae wakijua hivyo.

Wikienda: Lakini huoni kwamba ni tatizo kuzaa tena nje ya ndoa baada ya yule wa kwanza uliyezaa na bosi wa redio bila kufunga ndoa?

Hamisa: Hayo ni maisha yangu na kama nilivyosema, maneno ya watu hayanisumbui.
Hata hivyo, mazungumzo kati ya Wikienda na Hamisa yaliishia hapo kwa maelezo kwamba hataki tena kuulizwa jambo hilo kwani kila kitu kinajulikana.

MIMBA YA PILI?
Hii ni mimba ya pili ambayo Hamisa anadaiwa kupachikwa na msanii huyo baada ya ile ya awali aliyopachikwa mwaka jana kuchoropoka na kuwa gumzo kubwa baada ya mpenzi wa mwanaume huyo kuja juu na kuanzisha bifu ambalo halijawahi kuzimwa hadi leo.

STORI: IMELDA MTEMA NA MUSA MATEJA | IJUMAA WIKIENDA, DAR
Tayari klabu ya Everton  imethibitisha kumalizana na mshambuliaji wa Man United, Wayne Rooney kwa kumrejesha kwenye klabu hapo kwa mkataba wa miaka miwili.

Kupitia mtandao wa Klabu ya Everton taarifa zimesema wamefikia makubaliano hayo kwa mazungumzo ya muda mrefu na baada ya kutathmini uwezo wake na umri pamoja na uzalendo wake kwa klabu hiyo ambayo ndiyo imemkuza tangia akiwa na mika nane kabla ya kununuliwa na Man united mwaka 2004.

Dili la Manchester United kumchukua mshambuliaji wa Everton, Romelu  Lukaku limehusishwa pia na usajili wa nahodha huyo kipenzi cha mashabiki wa Man united, Wayne Rooney .

Tayari Rooney amekubali kujiunga na Everton kwa kupunguza mshahara wake wa wiki kutoka paundi 250,000 anazolipwa sasa na Manchester United mpaka 180,000 kiasi ambacho Everton wamekiri kukimudu.

Rooney kukubali kujiunga na Everton ni kujipatia tiketi ya kutembelea Tanzania kuja kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia alhamisi ya wiki lijalo (tarehe 13 julai).

Hii itakuwa fursa pekee kwa watanzania kumshuhudia nahodha huyo wa muda mrefu wa timu ya taifa ya England na klabu ya Manchester United kutua kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

Mwishoni mwa mwezi juni afisa utawala na utekelezaji wa kampuni ya SportPesa nchini Abbasi Tarimba alisema kuwa  klabu ya  Everton imethibitisha kuleta timu yake ya kikosi cha kwanza nchini tanzania kitu ambacho kinatupa uhakika kuwa huenda hata Rooney akaja Tanzania wiki ijayo.

Mtangazaji wa kituo cha redio cha E-Fm na Mwanamitandao ya kijamii, Seth Katende maarufu kama “Bikira wa Kisukuma” amefariki dunia Jumapili hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akitibiwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya EFM, Seth alifariki dunia baada ya kuugua ghafla kwa muda mrufi.
“Kwa masikitoko makubwa E FM inapenda kuwajulisha kuwa mwenzetu Seth Katende maarufu” Bikira wa kisukuma”amefariki dunia Leo mchana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili bmfupi. Seth atakumbukwa sana kwa ucheshi wake kupitia kipindi cha Ubaoni alichokua akiendesha sambamba na Imma Kapanga na Mpoki au “mwarabu wa Dubai”. Msiba upo nyumbani kwa baba yake mzazi Changanyikeni Dar es salaam.
Mmoja kati ya watangazaji wa EFM, Dina Marious ameeleza kusikitishwa na kifo hicho pamoja na neno la mwisho ambalo aliongea na marehemu kalba ya kifo chake.
“Tulikuwa wagonjwa wenza tumepishana wiki tu. Wewe umelazwa TMJ mimi nipo Sanitas kila siku lazima tuwasiliane tuchekiane vipi salama umeamkaje? kwemaa upande huo?Tupone bwana tukale firigisi,” aliandika Dina Instagram.
Aliongeza, “Simu yangu leo ilifichwa kwa muda nisielewe kinachoendelea wanaoniuguza wameuchuna mwisho ikabidi waseme tu.Kichwa kinaniuma sababu ya hali yangu lakini kimeongezeka maradufu kukulilia.Juzi unanipa moyo eti nitapona niende mtoto day Dah kumbe wewe hali imekuwa mbaya.#RIP SETH,”
Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi.
Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa ametembelea na kuzindua nyumba ya wahudumu wa afya katika kijiji cha Mkungo wilayani Chato mkoani Geita zilizojengwa na taasisi ya Mkapa Foundation kwa kushirikiana na Serikali.

Akizindua nyumba hizo jana, Rais Mkapa aliwasalimia wanachi kwa salam yake ya “mambo” na wananchi kuitika poa” na kuwataka kutunza nyumba hizo na kushirikiana vema na watumishi watakaoshi katika nyumba hizo kisha msafara wake kuondoka na kuelekea Ikulu ndogo iliyopo Chato.

Mkapa aliingia katika eneo la zahanati hiyo saa sita mchana akiongozana na mkewe, Mama Anna Mkapa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Uzinduzi wa nyumba hiyo ni ishara ya kuzindua nyumba nyingine 50 zilizopo katika mikoa ya Geita, Simuyu na Kagera .

Makabidhiano ya nyumba hizo yanatarajiwa kufanyika leo(Jumatatu July 10)  katika uwanja wa mpira wa miguu uliopo Chato mjini hafla itakayohudhuriwa na Rais John Magufuli.

Ofisa Mahusiano na Mawasiliano wa Mkapa Foundation, Deogratius Rimoy alisema nyumba 50 zilizojengwa na taasisi hiyo katika mikoa mitatu tofauti zimegharimu kiasi cha Sh 2.5 bilion

Alisema lengo la kujenga nyumba hizo ni ili kuboresha huduma za afya vijijini illi watumishi waweze kutoa huduma za afya kwa saa 24.

BAADA ya Jeshi la Polisi kumshikilia kwa zaidi ya saa 48 Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, ambaye ndiye chanzo cha kukamatwa kwa mwanasiasa huyo, amejivua kwenye sakata hilo.

Jana jeshi hilo lilimuhamisha Mdee kutoka katika mahabusu za Kituo cha Oysterbay alikokaa kwa siku nne na kumpeleka Kituo Kikuu cha Polisi (Central), ambako anaendelea kushikiliwa kwa kosa la uchochezi.

MTANZANIA Jumapili lilipomtafuta Hapi ili kufahamu kama amri ya saa 48 alizozitoa kwa polisi kumshikilia Mdee ina mabadiliko yoyote, alisema kwa sasa suala hilo asiulizwe yeye bali Jeshi la Polisi.

“Muulizeni Kaimu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,” alisema Hapi bila kufafanua.

MTANZANIA Jumapili lilipomtafuta Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya na kumuuliza kuhusu hilo, alijibu kuwa yuko likizo.

“Niko likizo, sijui kama (Mdee) yupo hapo, mtafute Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala,” alisema Mkondya.

Alipotafutwa kwa simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni, alikiri kuwa ni kweli mbunge huyo alipelekwa hapo kwa mahojiano.

“Aliletwa hapa kwa mahojiano, lakini ni suala la Kanda Maalumu,” alisema Kamanda Hamduni.

Alipoulizwa msingi wa mahojiano hayo, Kamanda Hamduni alisema kuwa hilo ni suala la kipelelezi kupitia Kanda Maalumu.

“Mimi si mpelelezi, anayepeleleza ni Kanda Maalumu,” alisema.

Mdee ambaye alihojiwa kwa saa kadhaa jana mara tu baada ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi, hakupatiwa dhamana kwa kile kilichoelezwa askari waliopewa jukumu la kumuhoji hawakuwa na maelekezo mengine.

Awali, MTANZANIA Jumapili lilimtafuta Wakili wa Mdee, Hekima Mwasipu ambaye alifafanua kuwa mteja wake alihojiwa kwa kosa la uchochezi.

“Ni kweli alihamishiwa Kanda Maalumu leo (jana),” alisema Mwasipu.

MTANZANIA Jumapili lilitaka kufahamu sababu za Mdee kuhamishwa kutoka Kituo cha Oysterbay na kupelekwa Kanda Maalumu ambako ameendelea kushikiliwa licha ya saa 48 kupita, Mwasipu alisema hata yeye alihoji na kujibiwa kuwa ni suala la polisi kanda hiyo.

“Sababu za kumtoa kule na kumleta Kanda Maalumu sielewi ni nini, lakini ninachoweza kusema ni kwamba Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa kushirikiana.

“Ila kwa maelezo yao hata mimi nilipowahoji walijibu kwamba makosa hayo yako chini ya Kanda Maalumu, ni ‘special’ (maalumu), kesi ziko chini ya kanda hiyo,” alisema Mwasipu.

Alipoulizwa kuhusu hali ya mbunge huyo ambaye awali aligoma kula na suala la dhamana, Mwasipu alisema hivi sasa anakula na alihojiwa kwa takribani saa moja, lakini dhamana yake ilishindikana.

“Suala la kufikiswa mahakamani ama kutofikishwa mahakamani hilo ni suala lao polisi, lakini maelezo kaandika na tulifuatilia suala zima la dhamana ikawa ngumu.

“Walisema wao hawana maelekezo yoyote kuhusu dhamana, ni wale ambao walikuwa wanamsimamia Halima kuandika maelezo, hadi jioni hii walinipigia simu, kimsingi leo hatapata dhamana, labda kesho,” alisema Mwasipu.

Awali, waandishi wa MTANZANIA Jumapili walifika kituoni hapo, lakini walizuiwa getini baada ya kujitambulisha kwa madai kuwa Kaimu Kamanda wa Kanda Maalumu hakuwapo ofisini na wala hakukuwa na mtu mwingine aliyekuwapo ili kutoa taarifa kwa waaandishi wa habari na kutakiwa kusubiri nje ya eneo la kituo.

Wakiwa nje ya kituo hicho ambako walikaa kwa saa kadhaa, walishuhudia hali ya utulivu huku ukaguzi ukiendelea, huku baadhi ya watu waliosadikika kuwa wafuasi wa Chadema walizuiwa kuingia na kukaa kando kwa muda kabla ya kuondoka.

Mdee, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), alikamatwa Julai 4, mwaka huu, baada ya Hapi kutoa amri ya kushikiliwa kwa saa 48 kutokana na matamshi aliyodai kuwa ni ya kumkashifu Rais Dk. John Magufuli.

Matamshi hayo anadaiwa kuyatoa katika mkutano aliofanya na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni, Dar es Salaam.

Mdee alidaiwa kumkashifu Rais Magufuli kutokana na kuhoji baadhi ya kauli zake zikiwamo zile alizotumia wakati akitangaza kupiga marufuku wanafunzi wa kike wanaopata mimba kurejea shuleni.

Si hilo tu, Mdee pia alihoji kauli nyingine zinazotolewa na Rais Magufuli ambazo alidai kuwa zinakiuka misingi ya sheria.

NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO INGIA WWW.AJIRAYAKO.COM

Wapiganaji wa Al Shabab wenye asilia ya kisomali wamewachinja wakenya 9 katika kijiji cha Poromoko siku ya Jumamosi.


Kwa mujibu wa habari,polisi wameviambia vyombo vya habari kuwa washambuliaji hao wanahisiwa kuwa wameingia Kenya kupitia mpaka wa Kenya na Somalia.


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa nchi yake imepata majanga mawili kwa wakati mmoja kwani  Kenya bado ilikuwa inaomboleza kifo cha waziri Joseph Nkaissery.


Vilevile rais Kenyatta  amewaahidi wananchi kuwa nchi yake itaongeza mbinu za kulinda usalama wa raia wake.


Hata hivyo polisi wameongezwa kulinda zaidi mahala tokeo hilo lilipotokea.

mwigizaji maarufu nchini kwa jila la “Jackline Wolper” ama unaweza mwita “wolperstylish” ambaye hivi karibuni alikuwa kwenye majonzi mazito baada ya kuachwa na “Harmonize” anayetokea “Wcb”,
Wolper aaibisha sanaa ya “Bongo movie” baada ya kuonekana akiwa na serengeti boy yani mvulana mdogo anayejulikana kwa jina la “BROWN MAUZO””
Stori ilianzia instagramu baada ya post mfululizo kutoka kwa “WOLPER” akiwa na mpenziye huyo na akimficha sura yani kumuonesha nusunusu na kuandika maneno kama my #bff.
Utata ukaibuka baada ya msichana anayekwenda kwa jina la “”sharonnbrown”” na kuandika maneno mazito kwenye comment ya moja ya post za wolper akiwa na huyo boy .
@Sharonnbrown” aliandika “soma comment yenye duara jekundu hapo chini.

Pamoja na hayo yote wolper na brounmauzo wazidi kula raha pasipo kuogopa maneno ya watu.
baadhi ya post za wolper akiwa na boy wake mpya.
1.Hiikutoka instagram ya wolper


Haya hapa maoni ya wadau na mashabiki wa wolper baada ya kuonekana akiwa na serengeti boy mwingine,Fuatana nasi…
Pia jicholauswazi.com tumekusogezea baadhi ya picha za huyu boy mpya wa WOLPERSTYLISH.
Unahisi wolper anafanya haya kwa ajili ya kumkomoa “””HARMONIZE”” au anafanya kwa matakwa yake???
usisahau kutembelea jicholauswazi.com kila siku kwa stori kama hizi

                                                                TAZAMA HII VIDEO



Mbunge wa Wilaya ya Iganga Grace Hailat Kaudha Magumba ameaga dunia.
Kaudha mwenye umri wa miaka 31, alifariki katika Hospitali ya Jiji la Kampala huko Kawempe, Kampala Jumamosi saa nane usiku. Alikuwa anaujauzito wa miezi mitano.
Kwa mujibu wa gazeti la Monitor Chris Obore, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa ofisi za Bunge amethibitisha hilo.
“Spika wa Bunge la Uganda Rebecca Kadaga anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Wilaya Igunga Kaudha Grace Hailat ambacho kimetokea jana usiku,” amesema Jumamosi.
“Tunatuma salamu za rambirambi zetu kwa watu wa Busoga, wabunge na nchi nzima kwa kumpoteza kiongozi huyu. Maandalizi ya maziko yatatangazwa hapo baadae,” Obore alisema.
Lakini gazeti la Daily Monitor limesema limepata taarifa kuwa marehemu atazikwa siku ya Jumamosi, Julai 8, saa kumi jioni katika kijiji cha Magogo, Iganga.
Matarisho ya maziko yatafanyika huko katika shule ya msingi ya manispaa ya Iganga.
Jumamosi ya July 8 2017 kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka Tanzania TFF ilikutana kwa mara ya kwanza baada ya kuvunjwa na kuundwa upya na kikao cha kamati ya utendaji ya TFF.

Baada ya kikao kumalizika na kufanya usahili wa wagombea wa nafasi zote na kuchuja, orodha ya wagombea waliyochujwa nafasi ya Urais ni pamoja na Rais wa sasa wa TFF Jamal Malinzi ambaye ameondolewa kwa sababu yuko Rumande

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi ya kuzalisha umeme wa Kinyerezi II na kusema kwamba ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wake.

Amesema hayo jana (Jumamosi, Julai 08, 2017) alipotembelea mradi huo wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia unaojengwa eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu alisema kukamilika kwa mradi huo kutaliwezesha Taifa kuwa na umeme wa uhakika, utakaowezesha kuendesha viwanda.

Alisema mkakati wa Serikali ni kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme ili Watanzania wapate umeme mwingi utakaosambazwa hadi vijijini kwa gharama nafuu.

“Tunataka tupate umeme wa kutosha ili viwanda vitakavyojengwa viwe na nishati ya uhakika na ya gharama nafuu. Ni wajibu wetu kuendelea kuimarisha utekelezaji wa miradi hii.” Alisema.

Naye, Meneja wa Mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi, Mhandisi Stephen Manda alisema gharama za mradi wa Kinyerezi II ni dola milioni 344.

Meneja huyo alisema tayari mradi huo umefikia asilimia 66.32 ya ujenzi wake na sasa wako katika hatua mbalimbali za kukamilisha, ikiwemo ujenzi wa misingi ya mitambo na jengo la kuendeshea mitambo.

“Pia tunaendelea na ujenzi wa nguzo za kupokelea laini ya msongo wa kilovoti 220 kutoka Kinyerezi I hadi Kinyerezi II, ambapo mtambo wa kwanza wa megawati 30 utawashwa ifikapo Desemba 2017 na kila mwezi tutaingiza megawati 30 katika gridi ya Taifa.”

Alisema miradi iliyoko katika eneo hilo ambayo iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji ni Kinyerezi 1 (150MW), Kinyerezi I Extension (185MW ) na Kinyerezi II (240MW).

Mhandisi Manda aliongeza kuwa mradi wa Kinyerezi 1 (150MW) ulikamilika Machi 2015 na miradi mwili ya Kinyerezi 1-extension na Kinyerezi II inatarajiwa kukamilika mwaka 2018.

Mhandisi Manda alisema miradi mingine inayotarajiwa kujengwa katika eneo hilo ni wa Kinyerezi III (600 MW) na Kinyerezi IV utakaozalisha (450 MW).

Awali Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda alisema mradi huo umewanufaisha wananchi wengi wa eneo hilo.

Alisema hadi sasa wananchi 100 wa eneo la Kinyerezi wameajiriwa katika miradi hiyo ambapo ni sawa na asilimia 40 ya watumishi wote.

Bi. Sophia alisema mbali na ajira pia wananchi wa eneo hilo watanufaika kwa kuboreshewa huduma mbalimbali za kijamii katika eneo hilo zikiwemo za maji na elimu ambapo wameahidiwa kupewa madawati ya shule tano